
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
United Nations
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Location:
New Rochelle, NY
Genres:
News & Politics Podcasts
Networks:
United Nations
Description:
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Twitter:
@HabarizaUN
Language:
Swahili
Contact:
9178215291
Episodes
Masuala ya watu wenye ulemavu ni lazima yapewe nafasi kimataifa: Jakeel D. Abdullah
6/11/2025
Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18, kinaendelea na mwaka huu, mada kuu ni kuongeza uelewa wa haki na mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya kijamii. Miongoni mwa washiriki ni ya kijana kutoka Louisiana, hapa Marekani. Je amesema nini? Flora Nducha na taarifa zaidi
Duration:00:01:59
Akili Mnemba (AI) au teknolojia inaweza kuwasaidia watu wenye ulemavu – Bongani Simphiwe Makama
6/11/2025
Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu Wenye Ulemavu – COSP18 – kinaendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ikiangazia juhudi za kimataifa za kuhakikisha usawa na ujumuishaji kwa watu wenye ulemavu. Miongoni mwa washiriki ni Bongani Simphiwe Makama mwakilishi wa watu wenye ulemavu kutoka Ufalme wa Eswatini, ambaye amepata nafasi ya kuzungumza na Idhaa ya Kiswahili kuhusu uzoefu wake, yale aliyojifunza, na changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini kwake. Sharon Jebichii na Makala zaidi.
Duration:00:03:49
11 JUNI 2025
6/11/2025
Hii leo jaridani tunaangazia ajali mbayá ya meli katika pwani ya Djibouti lililokuwa linabeba wahamiaji wengi. Pia tunasalia hapa makao makuu ambapo Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18. Mashinani tutakwenda nchini DRC.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM) kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka za Djibouti, linaongeza juhudi zake za kibinadamu kufuatia tukio la kusikitisha lililotokea pwani ya Djibouti ambapo takriban wahamiaji wanane walikufa maji na wengine 22 hawajulikani walipo.Katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18, kinaendelea na mwaka huu, mada kuu ni kuongeza uelewa wa haki na mchango wa watu wenye ulemavu katika maendeleo ya kijamii. Miongoni mwa washiriki ni ya kijana kutoka Louisiana, hapa Marekani.Makala tutasalia hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa New York Marekani ambapo Kikao cha 18 cha Nchi Wanachama wa Mkataba wa Haki za Watu wenye Ulemavu COSP18, kinaendelea na tutamsikiliza mmoja wa washiriki wa mkutano huu Bongani Simphiwe Makama kutoka Ufalme wa Eswatini ambaye amepata nafasi ya kuzungumza na idhaa ya Kiswahili.Na katika mashinani fursa ni yake fursa ni yake Byamungu Rukera, Mwakilishi wa watu waliokimbia makazi yao huko Sake, Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC akipazia sauti wakimbizi wenzake kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu na misaada ya dharura OCHA ambao wanawagawia chakula licha ya uhaba wa msaada huo.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:09:59
IOM yachukua hatua za dharura baada ya wahamiaji kufa maji katika pwani ya Djibouti
6/11/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji, (IOM) kwa ushirikiano wa karibu na mamlaka za Djibouti, linaongeza juhudi zake za kibinadamu kufuatia tukio la kusikitisha lililotokea pwani ya Djibouti ambapo takriban wahamiaji wanane walikufa maji na wengine 22 hawajulikani walipo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Duration:00:01:52
10 JUNI 2023
6/10/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayotupeleka katika ukanda wa Gaza, huko mashariki ya Kati kwenye eneo la Palestina lialokaliwa kimabavu na Israeli ambapo vinazidi kuibua changamoto mpya kila uchao.Changamoto ya uzazi duniani si kuhusu watu kukataa kuwa wazazi ni kuhusu kunyimwa fursa ya kuchagua kuwa mzazi imesema ripoti mpya ya shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu na afya ya uzazi UNFPA iliyotolewa leo na kuonesha kuwa kuwa matatizo ya kiuchumi, ukosefu wa usawa wa kijinsia, na hofu kuhusu maisha ya baadaye vinawazuia mamilioni ya watu kupata familia wanazotamani.Tishio la baa la njaa linaendelea kuiandama Sudan iliyoharibiwa vibaya na vita, limeonya leo Shirika laUmoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP, likitoa wito wa dharura kwa jamii ya kimataifa kusaidia kukidhi mahitaji yanayoongezeka na kuzuia maafa zaidi ya kibinadamu.Kwa mara ya kwanza dunia inaadhimisha siku ya kimataifa ya Mazungumzo baina ya Ustaarabu tofauti yenye lengo la kuchagiza amani, maelewano na mshikamano katika ulimwengu wa sasa uliogubikwa na chuki na mizozo.Na katika mashinani fursa ni yake Maria “Mãezinha” Sábado de Horta Fidalgo, Rais wa Ushirika wa wavuvi wadogo wa samaki katika kijiji cha Rincão kilichoko kisiwa cha Santiano nchini Cabo Verde barani Afrika anaelezea jinsi wanakabiliana na uhaba wa samaki kwenye eneo lao, na hii ni kutokana na mradi wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs unaotekelezwa na mashirka ya Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:10:50
UNEP inashirikiana na taifa la Tanzania kupambana na taka za plastiki - Clara Makenya
6/9/2025
Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataiifa kuhusu Bahari UNOC3 ukiendelea mjini Nice, Ufaranzsa, tunakuletea mahojiano kati ya Nafisa Didi afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam na Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, wakimulika mchango wa UNEP katika kuzisaidia nchi kupambana na taka za plastiki ambayo ni mada kuu ya mkutano wa UNOC3.
Duration:00:06:43
Mustakabali wa bahari u mikononi mwetu sisi tunaoiharibu - UN
6/9/2025
Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung’unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini. Assumpta Massoi amefuatilia na kuandaa taarifa hii.
Duration:00:02:22
09 JUNI 2025
6/9/2025
Hii leo jaridani tunaangazia Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa, na masuala ya baharini ikiwa ni pamoja na uvuvi nchini Sao Tome, umuhimu wa kutunza mazingira nchini Kenya na uondoaji wa taka za plastiki Tanzania.Mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu bahari umeanza leo huko Nice nchini Ufaransa ambapo Katibu Mkuu wa Umoja huo António Guterres bila kumung’unya maneno ameelezea bayana jinsi binadamu anavyozidi kuhatarisha ustawi wa bahari lakini akionesha matumaini ya hali bora ya bahari iwapo hatua zitachukuliwa kwa maslahi ya binadamu na viumbe vya baharini.Nchini São Tomé na Príncipe, nchi ya visiwa viwili vidogo huko Afrika ya Kati, mpango wa FISH4ACP unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO unalenga kusaidia wavuvi na wauzaji samaki hasa wanawake na vijana kuongeza kipato na manufaa ya kijamii kwa njia endelevu huku wakipunguza athari mbaya kwa makazi ya asili na viumbe wa baharini. Paola Afè Do Espiritu Afonso ni miongoni mwa wanawake wanaonufaika.Makala, tunasalia na mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataiifa kuhusu Bahari UNOC3, tunakuletea sehemu ya mwisho ya mahojiano kati ya Nafisa Didi afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam na Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, wakimulika mchango wa UNEP katika kuzisaidia nchi kupambana na taka za plastiki ambayo ni mada kuu ya mkutano wa UNOC3.Na katika mashinani fursa ni yake Kaara Waithaka, Mwanamazingira kutoka kaunti ya Kajiado nchini Kenya ambaye kupitia mahojiano yaliyofanikishwa na washirika wetu Radio Domus anatoa wito kwa vijana kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:11:01
São Tomé na Príncipe: Viumbe wa bahari, samaki, ni chanzo cha mapato, kuinua jamii na kuondoa umaskini
6/9/2025
Nchini São Tomé na Príncipe, nchi ya visiwa viwili vidogo huko Afrika ya Kati, mpango wa FISH4ACP unaoendeshwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO unalenga kusaidia wavuvi na wauzaji samaki hasa wanawake na vijana kuongeza kipato na manufaa ya kijamii kwa njia endelevu huku wakipunguza athari mbaya kwa makazi ya asili na viumbe wa baharini. Paola Afè Do Espiritu Afonso ni miongoni mwa wanawake wanaonufaika, Sharon Jebichi na maelezo zaidi.
Duration:00:02:00
Jifunze Kiswahili: maana ya neno KIHEREHERE
6/5/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno KIHEREHERE.
Duration:00:00:44
05 JUNI 2025
6/5/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo leo ikiwa ni siku ya mazingira duniani mwaka ikibeba maudhui “Tokomeza taka za Plastiki,” tunakwenda Tanzania kumsikia Clara Makenya, Mkua wa UNEP nchini humo na afisa mawasiliano wa shirika hilo kwa ajili ya Namibia akizungumza kuhusu changamoto ya taka za plastiki Tanzania na nini kifanyike kuzitokomeza.Naanzia hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani ambapo leo kumefanyika tukio maalum la kukumbuka na kuenzi watumishi 168 wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha wakitekeleza majukumu yao ya ulinzi wa amani, haki, na usaidizi, Mishumaa iliwashwa na kisha walitajwa majina yao mmoja baada ya mwingine akiwemo Nats.. mlinda amani wa UN kutoka Tanzania. Wanafamilia walipokea tuzo maalum za kutambua mchango wao.Leo ikiwa ni siku ya kimataifa ya mazingira, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ametaka hatua za dharura kutokomeza janga la uchafuzi utokanao na taka za plastiki, akilitaja kama “janga” linaloikaba dunia na kutishia afya ya binadamu, mifumo ya ikolojia, na hali ya hewa. Guterres amesema, kadri plastiki zinavyovunjika na kuwa vipande vidogo vidogo zinaingia kila mahali: kuanziaubongo wa binadamu hadi maziwa ya mama.Huko nchini Tanzania hii leo kwenye Chuo Kikuu Mzumbe mjini Morogoro, kumefanyika kongamano kumulika uhaba wa maji na sera bora zinazoweza kufanikisha upatikanaji wa huduma hiyo, kongamano lililoandaliwa kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP na Muungano wa Ulaya. Dkt. Saida Fundi Mhadhiri Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu Mzumbe anasema.Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "KIHEREHERE!.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Duration:00:11:03
Uwekezaji sahihi ni ule unaoanzia kwa wananchi na si ngazi ya juu - Madina
6/4/2025
Mkutano wa siku mbili kuhusu Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya dunia endelevu umekunja jamvi huko Hamburg nchini Ujerumani ambako Balozi wa Mabadiliok ya Tabianchi wa Vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania, Madina Jubilate Kimaro ameshiriki.
Duration:00:02:01
04 JUNI 2025
6/4/2025
Hii leo jaridani tunaangazia haki za jamii za Ogiek nchini Kenya, na masuala ya baharí na tabianchi. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kulikoni?Mtaalamu wa UN ataka kusitishwa mara moja kwa uwekaji mipaka unaotishia haki za Waogiek Kenya. Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa ameitaka Serikali ya Kenya kusitisha mara moja shughuli za uwekaji mipaka katika Msitu wa Mau Mashariki nchini humo, akisema kuwa unakiuka haki za jamii ya asili ya Waogiek na kupuuza maamuzi ya lazima ya Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR).Mkutano wa siku mbili kuhusu Ubia wa Kimataifa kwa ajili ya dunia endelevu umekunja jamvi huko Hamburg nchini Ujerumani ambako Balozi wa Mabadiliok ya Tabianchi wa Vijana wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF nchini Tanzania, Madina Jubilate Kimaro ameshiriki. Akiwa huko Hamburg nimemuuliza Madina ni kipi amejulisha washiriki wenzake kuwa kinapaswa kufanyika ili dunia iwe endelevu?.Makala, katika kuelekea mkutano wa tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari (UNOC3) utakaofanyika mjini Nice, Ufaransa, kuanzia tarehe 9 hadi 13 Juni 2025 ukijikita na maudhui "Kuharakisha hatua na kuhamasisha wadau wote kuhifadhi na kutumia bahari kwa njia endelevu", tunaelekea nchini Tanzania kwa Clara Makenya Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP nchini humo na afisa mawasiliano wa shirika hilo kwa ajili ya Namibia, akizungumza na kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa nchini Tanzania UNIC Dar es salaam anaeeleza nini kinapaswa kufanywa na jamii ya kitaifa na kimataifa ili kutekeleza azma ya mkutano huo.Na katika mashinani Debora, mkazi wa Sake jimboni Kivu Kaskazini, mashariki mwa DRC, aliyekimbilia mji wa Goma jimboni humo humo kutokana na machafuko sasa amerejea tena Sake ambako wanapatiwa msaada wa chakula kutoka shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP. Akisema PAM anamaanisha WFP.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:09:59
Kuelekea Mkutano wa Bahari UNOC3, UNEP yatoa wito wa hatua za kukabili taka za plastiki
6/4/2025
Katika kuelekea Mkutano wa Tatu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Bahari UNOC3, utakaofanyika mjini Nice, Ufaransa kuanzia tarehe 9 hadi 13 Juni 2025, Ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP nchini Tanzania imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na madhubuti kukabiliana na changamoto ya uchafuzi wa bahari, hasa wa taka za plastiki. Akizungumza na Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa nchini humo UNIC jijini Dar es Salaam, Clara Makenya, Mkuu wa Ofisi ya UNEP nchini Tanzania na Afisa Mawasiliano wa shirika hilo kwa Namibia, alisisitiza umuhimu wa kushughulikia kwa haraka tatizo la taka za plastiki ambazo nyingi hutokea nchi kavu na kuishia baharini.
Duration:00:03:23
Mtaalamu wa UN ataka kusitishwa mara moja kwa uwekaji mipaka unaotishia haki za Waogiek nchini Kenya
6/4/2025
Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa ameitaka Serikali ya Kenya kusitisha mara moja shughuli za uwekaji mipaka katika Msitu wa Mau Mashariki nchini humo, akisema kuwa unakiuka haki za jamii ya asili ya Waogiek na kupuuza uamuzi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR). Anold Kayanda na maelezo zaidi.
Duration:00:01:52
03 JUNI 2025
6/3/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kinainayomulika kilimo kinachohimili mabadiliko ya tabianchi katika kaunti kama Kajiado, Kenya, ambayo jamii hukumbwa na hali ya ukame na mazingira magumu, mabadiliko chanya yanaonekana.Mustakabali wa mzingiro wa Israeli kwenye eneo la Palestina la Gaza inalokalia kimabavu ukiendelea kukumbwa na sintofahamu, wanawake na wasichana wamesimulia adha ya ukosefu taulo za kike wakati wanapokuwa kwenye hedhi huku upatikanaji wa maji ukiwa ni wa taabu.Idadi ya wakazi wa nchi zenye maendeleo duni, LDCs na zile za visiwa vidogo, SIDS wanaopata huduma zilizoboreshwa au za kisasa za maonyo ya mapema kabla ya majanga imefikia takribani milioni 400 na hii ni kutokana na programu ya CREWS iliyoanzishwa mwaka 2015 na shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO.Rebecca Kalonji, al maaruf Sista Becky, mwimbaji chipukizi wa mtindo wa kufokafoka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hii leo ametangazwa kuwa Muungano Mkono wa Ngazi ya Juu wa masuala ya lishe na ulaji wenye afya wa shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP katika taifa hilo la Maziwa Makuu. Watu milioni 28 wakikabiliwa na njaa kali nchini mwake, Sista Becky amesema atatumia sauti na kazi yake kupatia vijana changamoto ya sio tu kupaza sauti zao bali pia kuchukua hatua kwenye masuala nyeti yanayogusa mustakabali wao ikiwemo kupata lishe bora na fursa bora kwa wanawake na Watoto wa kike.Na katika mashinani fursa ni yake Christiana, mama wa watoto sita ambaye ni mwathirika wa mashambulizi ya hivi majuzi ya waasi wenye silaha katika wilaya za Mirebalais na Saut-d'Eau yaliyosababisha watu wengi kuyahama makazi yao. Anasema ana matumaini kwani Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF limewapelekea huduma za afya kupitia kniki tembezi.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:10:46
Shirika la kiraia lawezesha vijana wa kike kujiajiri badala ya kutumbukia kwenye umaskini
6/2/2025
Nchini Tanzania ugumu wa maisha na kukabiliwa na vishawishi, umewapa fikra mpya vijana wa kike mkoani Morogoro, mashariki mwa taifa hilo la Afrika Mashariki, ambao sasa wanajimudu kiuchumi, kwa kuanzisha biashara na shughuli za ujasiriamali. Wanasongesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs hususan namba 8 la ajira zenye staha, nan amba 1 la kutokomeza umaskini. Hamad Rashid wa Redio washirika Tanzania Kids Time FM amewatembelea vijana hao na kuandaa makala hii.
Duration:00:03:36
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ashutumu mashambulizi dhidi ya Wapalestina wanaotafuta msaada
6/2/2025
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza kughadhabishwa kufuatia kusambuliwa, kujeruhiwa na kuuawa kwa Wapalestina walipokuwa wakijaribu kupata msaada wa kibinadamu huko Gaza jana Jumapili, Juni Mosi. Selina Jerobon na taarifa zaidi.
Duration:00:01:49
02 JUNI 2025
6/2/2025
Hii leo jaridani tunaangazia haki za kibidamu katika ukanda wa Gaza, na hali ya misaada ya kibinadamu huko huko Gaza. Makala yunakwenda nchini Tanzania kusikia harakati za kusaidia vijana wa kike, na mashinani tunakupeleka nchini Uganda kusikia kuhusu mradi wa mlo shuleni.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameeleza kughadhabishwa kufuatia kusambuliwa, kujeruhiwa na kuuawa kwa Wapalestina walipokuwa wakijaribu kupata msaada wa kibinadamu huko Gaza jana Jumapili, Juni Mosi.Maisha ya raia wa Gaza ambao karibu wote ni wakimbizi wa ndani yanazidi kuwa mtihani usio na majawabu kila uchao kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Mateso wanayopitia nis awa na kuishi jrehanamu, wengi wamekata tamaa na wanaona bora kufa kuliko kuishi katika hali hiyo. Flora Nducha akusimulia madhila ya mmoja wa wakimbizi hao wa ndani Moamen Abu Asr na mkewe Zeinat.. Makala inakupeleka nchini Tanzania kusikia harakati za kunasua vijana wa kike kutoka vishawishi vinavyoweza kuwatumbukiza kwenye lindi la umaskini. Msimulizi wako ni Hamad Rashid wa Radio washirika Tanzania Kids Time FM.Na katika Moses Okiror, Naibu Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Rainbow iliyoko Karamoja kaskazini-masharikimwa Uganda anaeleza jinsi Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula (WFP) limeboresha mpango wa mlo shuleni kwa kuwakabidhi mashine ya kusagisha nafaka aina mbalimbali yenye vinu vinavyotumia nishati ya jua.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:11:06
Tumefika mwisho, ni bora kufa kuliko mateso haya: Wakimbizi Gaza
6/2/2025
Maisha ya raia wa Gaza ambao karibu wote ni wakimbizi wa ndani yanazidi kuwa mtihani usio na majawabu kila uchao kwa mujibu wa mashirika ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa. Mateso wanayopitia nis awa na kuishi jrehanamu, wengi wamekata tamaa na wanaona bora kufa kuliko kuishi katika hali hiyo. Flora Nducha akusimulia madhila ya mmoja wa wakimbizi hao wa ndani Moamen Abu Asr na mkewe Zeinat.
Duration:00:02:53