
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
United Nations
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Location:
New Rochelle, NY
Genres:
News & Politics Podcasts
Networks:
United Nations
Description:
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Twitter:
@HabarizaUN
Language:
Swahili
Contact:
9178215291
Episodes
Ukame unavyobadili ratiba ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama
8/6/2025
Bado dunia ikiendelea kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Kelvin Keitany wa Radio Washirika, Domus Radio iliyoko huko Kajiado, eneo linalokabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile ukame, anamulika ni kwa jinsi gani madhara hayo yanakwamisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama miezi sita ya mwanzo ya uhai bila kitu chochote, Je hali iko vipi Kajiado. Kelvin Keitany na maelezo zaidi.
Duration:00:02:33
06 AGOSTI 2025
8/6/2025
Jaridani hii leo tunaangazia suala la afya katika ukand wa Gaza, na wito wito wa Umoja wa Mataifa wa kutaka kuachiliwa huru kwa mateka wa Israeli huko Gaza. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani nchini Tanzania, kulikoni?Ikiwa ni siku 668 tangu Hamas ambao ni wanamgambo wa kipalestina wateke waisraeli 250 baada ya kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati, vuta nikuvute ilikuwa bayana kwenye Baraza la Usalama baada ya kikao cha dharura kuitishwa na Israeli kufuatia kuchapishwa kwa picha za mateka wawili walio hoi bin taaban.Leo tuna habari njema kutoka Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Mashariki ya Kati, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na Umoja wa falme za Kiarabu UAE wamefanikiwa kuingiza dawa, vifaa tiba na damu salama kwa ajili ya matibabu ya wanagaza ambao wanaendelea kuteseka na madhila ya vita. Makala inakupeleka nchini Kenya, hususan kaunti ya Kajiado. Bado dunia ikiendelea kuadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, Kelvin Keitany wa Radio Washirika, Domus Radio iliyoko huko Kajiado, eneo linalokabiliwa na madhara ya mabadiliko ya tabianchi, kama vile ukame, anamulika ni kwa jinsi gani madhara hayo yanakwamisha unyonyeshaji wa mtoto maziwa ya mama. Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO limetoa mwongozo mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama miezi sita ya mwanzo ya uhai bila kitu chochote, Je hali iko vipi Kajiado.Na mashinani fursa ni yake Dkt. Beatrice mwilike, Mkunga Bingwa na Rais wa Chama cha wakunga Tanzania (TAMA) ambaye kupitia mradi unaolenga uzazi salama kwa watoto milioni 10 ifikapo 2030 lililozinduliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ya Uzazi na Idadi ya Watu, UNFPA kwa kusaidiana na serikali ya Denmark, anasema wakunga wanatumia appu na njia za kisasa zinazowapa taarifa sahihi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:09:59
Umoja wa Falme za Kiarabu wafanikisha vifaa vya matibabu ikiwemo damu kuwasili Gaza
8/6/2025
Leo tuna habari njema kutoka Gaza, eneo la palestina linalokaliwa kwa mabavu na Israel huko Mashariki ya Kati, Shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni WHO kwa kushirikiana na Umoja wa falme za Kiarabu UAE wamefanikiwa kuingiza dawa, vifaa tiba na damu salama kwa ajili ya matibabu ya wanagaza ambao wanaendelea kuteseka na madhila ya vita. Leah Mushi na taarifa zaidi.
Duration:00:02:11
UN yarejelea wito wa kutaka kuachiliwa huru kwa mateka wa Israeli huko Gaza
8/6/2025
Ikiwa ni siku 668 tangu Hamas ambao ni wanamgambo wa kipalestina wateke waisraeli 250 baada ya kushambulia taifa hilo la Mashariki ya Kati, vuta nikuvute ilikuwa bayana kwenye Baraza la Usalama baada ya kikao cha dharura kuitishwa na Israeli kufuatia kuchapishwa kwa picha za mateka wawili walio hoi bin taaban. Anold Kayanda na tarifa zaidi.
Duration:00:01:51
05 AGOSTI 2025
8/5/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambayo inamulika unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama, uwekezaji kwenye mustakabali yao, kauli mbiu ya Wiki ya unyonyeshaji duniani iliyoanza tarehe Mosi mwezi huu wa Agosti na itakunja jamvi tarehe 7.Mashirika ya Umoja wa Mataifa lile la Wanawake, UN Women na la watoto, UNICEF yamewaeleza waandishi wa habari jijini Geneva Uswisi kuwa hali ya njaa Sudan inazidi kuwa kali zaidi. Salvator Nkurunziza, Mwakilishi wa UN Women Sudan amesema kwamba UN Women inashauri zipewe kipaumbele kaya zinazoongozwa na wanawake, pamoja na makundi kama wanawake wajawazito, wanaonyonyesha, na wasichana balehe katika kila aina ya msaada wa chakula.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres leo katika ufunguzi wa Mkutano kuhusu nchi zisizo na Bahari LLDC3 unaofanyika Awaza, Turkmenistan amewasihi viongozi kufikiria upya maendeleo kwa mataifa yasiyo na bahari akisema, “leo tunakusanyika hapa kuthibitisha ukweli kwamba jiografia haipaswi kamwe kuamua hatima ya nchi.” Tukirejea Geneva, Uswisi unakofanyika mkutano utakaweka mwelekeo wa jinsi ya kukabiliana na uchafuzi unaotokana na plastiki duniani, Inger Andersen, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Mazingira Duniani, UNEP, ameonya kwamba, “uchafuzi wa plastiki tayari upo katika mazingira, baharini, na hata katika miili yetu. Tukizidi kuendelea kwa mwelekeo huu, dunia yote itazama katika uchafuzi wa plastiki.”Na mashinani leo tuko katika shoroba za makao makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani ambapo wageni hutoka kila pembe ya Dunia kutembelea jengo hili la kihistoria. Mwalimu Maria Rulands ni mmoja wao.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:10:51
Kituo kipya cha kikanda cha SDGs Asia chazinduliwa Kazakhstan
8/4/2025
Umoja wa Mataifa na Kazakhstan wamesaini makubaliano ya Kazakhstan kuwa mwenyeji wa Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa ajili ya ukanda wa Asia ya Kati na Afghanistan. Anold Kayanda anafafanua zaidi.
Duration:00:03:10
Raia wanaendelea kuuawa katika ukanda wa Gaza wakihaha kusaka chakula
8/4/2025
Simulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula. Simulizi zaidi anayo Assumpta Massoi.
Duration:00:02:03
04 Agosti 2025
8/4/2025
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya msaada wa kibinadamu katika ukanda wa Gaza, na mlipuko wa kipindupingu nchini Sudan. Makala tunafuatilia ziara ya katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Kazakhstan na mashinani tunamulika unyonyeshaji Sudan Kusini.Simulizi za huzuni, majonzi na kukata tamaa zinaendelea kila uchao huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel hasa wakati huu ambapo raia wanaokwenda kusaka chakula wanakumbwa na mashambulizi yanayosababisha vifo. Ijumaa iliyopita Umoja wa Mataifa uliripoti kuwa zaidi ya watu 100 waliuawa na mamia kadhaa walijeruhiwa katika siku mbili pekee Wakisaka chakula.Zaidi ya watoto 640,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wapo hatarini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Kaskazini mwa Darfur, nchini Sudan.. Katika makala Anold Kayanda anatupeleka Asia ya Kati ambako Umoja wa Mataifa na Kazakhstan wamesaini makubaliano ya Kazakhstan kuwa mwenyeji wa Kituo cha Kikanda cha Umoja wa Mataifa cha Malengo ya Maendeleo Endelevu kwa ajili ya ukanda wa Asia ya Kati na Afghanistan..Na mashinani nawapisha wanafunzi wawili,Wanga pamoja na Kifaya ambao ni wanafunzi katika shule ya Sekondari ya Askofu Abangite iliyopo jimbo la Yambio,kusini Magharibi mwa Sudani Kusini karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.Wakizungumza na shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia watoto UNICEF nchini humo wameeleza umuhimu wa maziwa ya mama kwa mtoto.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:09:59
Watoto zaidi ya 640,000 wako hatarini kufuatia mlipuko wa kipindupindu Darfur
8/4/2025
Zaidi ya watoto 640,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano wapo hatarini kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu huko Kaskazini mwa Darfur, nchini Sudan. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Selina Jerobon
Duration:00:02:01
IMF yatoa mtazamo mpya wa Uchumi wa dunia kwa mwaka 2025/ 2026
8/1/2025
Mnamo mwezi April mwaka huu Shirika la Fedha la Kimataifa IMF lilitoa makadirio na mtazamano wa uchumi wa dunia ambapo lilieleza pamoja na mambo mengine kuongezeka kwa vikwazo vya biashara kunasababisha kushuka kwa kasi kwa ukuaji wa uchumi wa dunia mwelekeo ambao ulielezwa kuathiri nchi nyingi duniani.Tarehe 29 Julai IMF ikatoa ripoti mpya, ambapo tathmini mpya ya mwelekeo wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026 ikionesha matumaini tofauti na hali ilivyoonesha miezi mitatu mitatu iliyopita. Leah Mushi amefuatilia ripoti hiyo nakutuandalia makala hii akieleza kwa kina.
Duration:00:03:34
Ndoto ya Sahar ya kushamiri kimaisha yatwamishwa na mashambulizi ya Israeli Gaza
8/1/2025
Harakati za kila uchao kwa raia wa Gaza huko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli za kukimbilia chakula huku mashambulizi yakiendelea zimeendelea kusababisha vifo na majeruhi ambapo majeruhi wa hivi karibuni aliyetajwa ni Sahar, mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyepata ulemavu akikimbilia kupokea msaada wa chakula. Ripoti ya Selina Jerobon inayotokana na video iliyochapishwa mtandao wa X na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa kipaletina, UNRWA, inafafanua zaidi.
Duration:00:02:03
01 AGOSTI 2025
8/1/2025
Hii leo jaridani tunaangazia hali ya wakimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza, na mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi. Makala tunamulika mtazamo mpya wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026, na mashinani tunakwenda nchini Somalia, kulikoni.Harakati za kila uchao kwa raia wa Gaza huko eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli za kukimbilia chakula huku mashambulizi yakiendelea zimeendelea kusababisha vifo na majeruhi ambapo majeruhi wa hivi karibuni aliyetajwa ni Sahar, mtoto mwenye umri wa miaka 14 aliyepata ulemavu akikimbilia kupokea msaada wa chakula.Mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi, jana Julai 31 umefika tamati baada ya siku tatu za mijadala ambazo zimezaa Azimio la kihistoria linalotoa wito wa "ushirikiano wa kimataifa ulio thabiti na wenye ufanisi zaidi" ili kuendeleza amani, haki, na ustawi. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU), Tulia Ackson kupitia hotuba ya kufunga mkutano huo uliondaliwa kwa ushirikiano wa IPU na Umoja wa Mataifa akadokeza kilichomo katika azimio hilo. Katika makala Leah Mushi anatuletea habari njema kutoka shirika la fedha la kimataifa IMF kuhusu mtazamo mpya wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2025 na 2026.Na mashinani tutakupeleka nchini Ethiopia, kumulika harakati za kujikwamua kiuchumi katikati ya janga la ukame.Mwenyeji wako ni Assumpta, karibu!
Duration:00:10:49
Maspika wa Mabunge wapitisha azimio la kihistoria Geneva, Uswisi
8/1/2025
Mkutano wa Sita wa Maspika wa Mabunge Duniani uliofanyika jijini Geneva, Uswisi, jana Julai 31 umefika tamati baada ya siku tatu za mijadala ambazo zimezaa Azimio la kihistoria linalotoa wito wa "ushirikiano wa kimataifa ulio thabiti na wenye ufanisi zaidi" ili kuendeleza amani, haki, na ustawi. Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani, (IPU), Tulia Ackson kupitia hotuba ya kufunga mkutano huo uliondaliwa kwa ushirikiano wa IPU na Umoja wa Mataifa akadokeza kilichomo katika azimio hilo.
Duration:00:02:22
Fursa zipo, vijana wajitokeze kusongesha malengo ya maendeleo endelevu - Kapwani
7/31/2025
Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) lilifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani mwezi Aprili mwaka huu wa 2025. Jukwaa hili lilifanyika kwa siku 4 likileta pamoja vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani na wadau wa maendeleo na uchumi ili kujadili changamoto zinazowakabili vijana na kutoa mapendekezo ya kuboresha dunia kuelekea usawa na maendeleo endelevu chini ya Ajenda ya 2030 au Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).Miongoni mwa vijana walioshirikki ni Kapwani Kavenuke, kutoka Tanzania. Akizungumza na Sharon Jebichii wa Idhaa hii, Bi. Kapwani alianza kwa kuelezea alichokuwa anasongesha mbele baada ya kushiriki mkutano wa Zama Zijazo au Summit of The Future uliopitisha Mkataba wa Zama Zijazo au PACT OF THE FUTURE mwezi SEptemba mwaka jana 2024.
Duration:00:05:17
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno MTAGARUKI
7/31/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno MTAGARUKI.
Duration:00:00:52
31 JULAI 2025
7/31/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoturesha katika Jukwaa la Vijana la Baraza la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Kiuchumi na Kijamii (ECOSOC) lilifanyika katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York, Marekani mwezi Aprili mwaka huu wa 2025, ambapo Idhaa hii ilizungumza na Kapwani Kavenuke, kutoka Tanzania kuhusu ujumuishwaji wa vijana katika será za maendeleo.Nchini Somalia ziara ya siku nne ya Naibu Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM Ugochi Daniels imeonesha namna taifa hilo lilivyoathirika vibaya na mabadiliko ya tabianchi hali inayofanya baadhi ya watu kukimbilia maeneo yenye rasilimali chache na hivyo kujikuta wakigombania rasilimali hizo.Huko Gaza mashariki ya kati, eneo la Wapalestina linalokaliwa kimabavu na Israel bado hali si hali kwani njaa ni Kali. Wakati malori ya misaada yakiendelea kuingiza chakula, mafuta na vifaa vya matibabu, mfanyakazi mmoja wa Umoja wa Mataifa anasimulia kumuona baba mmoja wa makamo akiwa amepiga magoti chini akiokota kwa mikono yake na kuweka kwenye fulana yake dengu zilizokuwa zimeanguka kutoka kwenye moja ya malori yanayoingiza chakula Gaza, hii ndio hali halisi. Umoja wa Mataifa umelaani shambulio lililotekelezwa hii leo na majeshi ya Urusi katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv na kusababisha vifo vya watu kadhaa akiwemo mtoto mwenye umri wa miaka sita huku watu wengine kadhaa wakijeruhiwa..Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili. Onni Sigalla, Mhariri Mwandamizi kutoka Baraza la Kiswahili Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno MTAGARUKI.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!
Duration:00:09:56
Siku ya kimataifa ya urafiki, je wewe wapenda kuwa na rafiki wa aina gani?
7/30/2025
Umoja wa Mataifa kwa kutambua nafasi ya urafiki katika kujenga amani, utulivu na kusongesha maendeleo kuanzia ngazi ya mtu mmoja mmoja hadi ngazi ya mataifa, mwaka 2011 kupitia Baraza lake Kuu, ulitenga Julai 30 kuwa siku ya urafiki duniani. Umoja wa Mataifa unasema katika wakati ambapo kelele za mgawanyiko zinazidi kuwa kubwa — zikiendeshwa na vita, migogoro, ukosefu wa usawa, na hofu — urafiki unaonekana kuwa wa kishujaa kutokana na unyenyekevu wake. Urafiki huanza na kitu cha utulivu zaidi: mazungumzo, wakati wa pamoja, utayari wa kuonana si kama wageni bali kama wasafiri wenza katika safari ya utu. Je huko Kenya, mkazi mmoja wa Kaunti ya Kajiado, urafiki kwake ni nini? Kelvin Keitany wa Redio washirika Radio Domus amefunga safari na kutuandalia makala hii.
Duration:00:03:05
IFAD: Kilimo chazaa matunda Rwanda: wakulima wadogo wajikwamua
7/30/2025
Katika kijiji kimoja nchini Rwanda, ndoto ya muda mrefu ya Chantal Uwizeyimana imegeuka kuwa njia ya kujikwamua kiuchumi. Kupitia mradi wa STARLIT unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, wakulima wadogo kama Chantal wamepata mafunzo, pembejeo na maarifa ya kubadili kilimo kuwa chanzo cha mapato ya uhakika. Sasa si tu kwamba mavuno yameongezeka, bali pia maisha yamebadilika kwa namna isiyotarajiwa. Sharon Jebichii na taarifa zaidi.
Duration:00:02:07
30 JULAI 2025
7/30/2025
Hii leo jaridani tunaangazia hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi nchini Tanzania, na biashara ndogondogo kwa wananchi wa Rwanda. Makala tunakupeleka nchini Kenya ma Mashinani tunakwenda Geneva Uswisi, kulikoni?Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), iko mbioni kuzindua mpango wa “Beat the Heat” yaani “Lishinde Joto”, mpango wenye lengo la kukabiliana na joto kali na hatari za kimazingira katika sehemu za kazi na kwenye matukio makubwa ya kijamii. Anold Kayanda anafafanua zaidi taarifa iliyochapishwa leo na WHO jijini Dar es Salaam, Tanzania.Katika kijiji kimoja nchini Rwanda, ndoto ya muda mrefu ya Chantal Uwizeyimana imegeuka kuwa njia ya kujikwamua kiuchumi. Kupitia mradi wa STARLIT unaotekelezwa na Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Maendeleo ya Kilimo – IFAD, wakulima wadogo kama Chantal wamepata mafunzo, pembejeo na maarifa ya kubadili kilimo kuwa chanzo cha mapato ya uhakika. Sasa si tu kwamba mavuno yameongezeka, bali pia maisha yamebadilika kwa namna isiyotarajiwa. Makala inakupeleka Kenya kwake Kevin Keitany wa Radio washirika Radio Domus akimulika siku ya kimataifa ya urafiki inayoadhimishwa leo Julai 30, ikimulika urafiki katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, baina ya watu zaidi ya mmoja, jamii, tamaduni na hata mataifa na mchango wake katika amani na utulivu duniani. Kelvin anamulika urafiki kati ya watu wawili.Na katika mashinani tuelekee jijini Geneva, Uswisi ambako unafanyika Mkutano wa Sita wa Spika wa Mabunge Duniani kumsikia Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani akitoa wito kwa viongozi wenzake kuutetea Umoja wa Mataifa.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:09:58
Tanzania kuanza kutekeleza mpango wa WHO wa Beat the Heat
7/30/2025
Tanzania, kwa kushirikiana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO), iko mbioni kuzindua mpango wa “Beat the Heat” yaani “Lishinde Joto”, mpango wenye lengo la kukabiliana na joto kali na hatari za kimazingira katika sehemu za kazi na kwenye matukio makubwa ya kijamii. Anold Kayanda anafafanua zaidi taarifa iliyochapishwa leo na WHO jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Duration:00:01:49