Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu-logo

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

United Nations

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Location:

New Rochelle, NY

Description:

Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twitter:

@HabarizaUN

Language:

Swahili

Contact:

9178215291


Episodes
Ask host to enable sharing for playback control

Askari watoto waachiliwa Sudan Kusini

10/20/2025
Sudan Kusini yaahidi kutotumikisha tena watoto jeshiniHuko nchini Sudan Kusini barani Afrika, matumaini mapya yamechipua baada ya watoto waliokuwa wametumikishwa kwenye jeshi la nchi hiyo, SSPDF kuachiliwa rasmi katika hafla iliyoungwa mkono na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, UNMISS. Tukio hilo limeelezwa kuwa ishara muhimu ya kumaliza utumikishaji wa watoto katika jeshi na kuwapa nafasi ya kujenga maisha mapya. Sabrina Saidi ana taarifa zaidi...(TAARIFA YA SABRINA SAIDI)Nats..Video ya UNMISS inaanzia kwenye tukio la viongozi wakikabidhi vifaa vya shule kwa watoto walioachiliwa kutoka jeshi la serikali.Nats..Ni siku ya matumaini hapa mjini Yambio, jimbo la Equatoria Magharibi nchini Sudan Kusini — siku ambayo watoto waliopoteza utoto wao vitani, sasa wanaupokea tena, wakiwa na ndoto mpya za elimu na maisha bora zaidi.Hafla ya makabidhiano iliyofanyika kwa ushirikiano kati ya Jeshi la serikali na Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (UNMISS), imeashiria azma ya serikali ya kuondokana na utumikishaji wa watoto jeshini.Brigedia Akech Maker, Kamanda wa Kikosi cha 16 cha SSPDF, anasema ….Clip- Sauti ya Brigedia Akech Maker“Hatutaruhusu watoto kujiunga na jeshi. Watoto wanaoonesha nia, tutawaelekeza kwenye elimu, na taasisi ziwaunge mkono ili wasirudi kambini.”Afisa wa Ulinzi wa Watoto UNMISS,, Rita Bampo, akatoa ahadi akisema watoto lazima warejee kwenye jamii, na kwamba…Clip- Sauti ya Rita Bampo“Tutahakikisha mchakato huu unafanikiwa na hakuna atakayewarudisha kwenye makundi ya kijeshi. Viongozi wote wahakikishe watoto wanapelekwa kwa mashirika yanayohusika."UNICEF pia imetoa huduma za kisaikolojia na vifaa vya kujifunzia kwa watoto hao, kuwasaidia kuanza upya safari yao ya elimu na matumaini.

Duration:00:01:46

Ask host to enable sharing for playback control

Warsha za UNDP Tanzania zaleta matokeo chanya

10/20/2025
Matunda ya warsha zilizokuwa zinaendeshwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, (UNDP) nchini Tanzania katika mikoa ya Tanga na Mtwara iliyoko kando mwa baharí ya Hindi kuhusu uchumi rejeshi yameanza kuonekana na mipango zaidi inafanyika ili matunda hayo yasambae mikoa mingine.Afisa wa UNDP Peter Nyanda ameiambia Idhaa ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni kuwa warsha hizo mbili zilizofanyika mwaka huu na kujumuisha vikundi vya kijamii na mamlaka za serikali za mitaa katika mikoa husika zililenga pamoja na mambo mengine kuhakikisha taka hasa taka ngumu hazitupwi bali zinarejeshwa katika mzunguko wa thamani kwa njia za ubunifu na endelevu.Nyanda anataja baadhi ya matokeo;(Sauti ya Peter Nyanda 1)“Ni kuwa na mpango wa utekelezaji katika kila mkoa ambao wadau hawa wanajiwekea ili kubainisha hatua za haraka, fursa na namna gani wanaweza kupata uwekezaji. Lakini pia tumeweza kuwatambua wadau katika uchumi rejeshi na pia tumeangalia wabunifu walioko kwenye maeneo ya viwanda. Kwa mfano tu kwa Mtwara tumefahamishwa hapa kwamba kiwanda cha Dangote tayari kinatumia taka katika kuwasha mitambo yake hasa . Lakini pia tunatarajia majadiliano pamoja na wafadhili na wadau wengine wa kimaendeleo hasa sekta binafsi katika kupata rasilimali za kufanya uwekezaji.”Akazungumzia pia matarajio ya baadaye ya UNDP kupitia warsha hizo akisema,(Sauti ya Peter Nyanda 2)“Ni kuanzisha vituo vya ubunifu na ubora katika ujenzi wa miundombinu, sio UNDP peke yake bali kwa ujumla, kama matarajio ya wadau. Lakini pia kuna wabunifu kama kuanzisha vituo vya kutenganisha taka. Lakini kufanikisha ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na taasisi za kifedha, ambao ni muundo wa utatu tunaojaribu kufanikisha kwa serikali, wadau na UNDP ikiwemo kuweza kuhakikisha mitaji inapatikana ili kuweza kusaidia kukuza biashara hizo. Kingine ni kupanua juhudi katika mikoa mingine sio tu ile ambayo mikoa mingine ya pwani ya sasa tunajua taka hizi za plastiki zinaathiri zaidi maeneo ya baharini.”Na hatimaye,(Sauti ya Peter Nyanda 3)“Ujumbe wangu wa mwisho ni kwamba uchumi rejeshi ni fursa ya kiuchumi, kiteknolojia na kimazingira. Kwa kuwekeza katika kurejesha thamani ya taka, tunalinda mazingira na wakati huo huo tunafungua ajira za ubunifu mpya kwa vijana na jamii yetu.”

Duration:00:03:01

Ask host to enable sharing for playback control

WMO na wadau wajadili kuhusu tahadhari za mapema

10/20/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa ka Utabiri wa Hali ya Hewa Duniani WMO linaongeza kasi ya jitihada za kulinda maisha ya watu dhidi ya madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mkutano wake Maalum uliofunguliwa leo mjini Geneva Uswisi, unalenga kuharakisha mpango wa kimataifa wa Tahadhari za Mapema kwa Wote, sambamba na maadhimisho ya miaka 75 ya WMO. Flora Nducha amefuatilia na anafafanua zaidi (TAAFIFA YA FLORA NDUCHA)Asante Leah, kwa mujibu wa WMO idadi ya nchi zenye mifumo ya tahadhari za mapema kwa ajili ya majanga ya tabianchi imeongezeka maradufu katika kipindi cha miaka kumi iliyopita lakini bado mamilioni ya watu hawana ulinzi dhidi yah atua hiyo muhimu.Ndiyo maana shirika hilo limewakutanisha mawaziri na wataalamu kutoka nchi wanachama 193 kuharakisha mpango wa Tahadhari za Mapema kwa Wote, uliozinduliwa mwaka 2022 na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres unatekelezwa kwa vitendo.Katika mkutano huo Celeste Saulo Katibu Mkuu wa WMO amesema “Miaka 75 iliyopita, Shirika la WMO lilianzishwa kutokana na ukweli kwamba hali ya hewa, maji na tabianchi havina mipaka ya kitaifa. Ushirikiano wa kimataifa katika uchunguzi na utabiri ni wa lazima, kwa sababu hakuna nchi inayoweza kufanya hivyo peke yake.”Ripoti mpya ya WMO, iliyopewa jina Tahadhari za Mapema kwa Wote Mtazamo wa Dunia, inaonesha kuwa licha ya maendeleo makubwa katika ubadilishanaji wa takwimu na utabiri wa kidijitali, bado kuna mapengo makubwa, hasa katika nchi maskini na visiwa vidogo vinavyoendelea.Celeste amesisitiza kuwa“Tahadhari za Mapema kwa Wote sasa siyo mpango tena, bali ni nembo ya mshikamano wa dunia. Pamoja, tunaokoa maisha, tunaunda sera, na kuimarisha mnepo.”Takwimu za shirika hilo zinaonesha uzito wa changamoto. Katika miaka 50 iliyopita, WMO inasema majanga yanayohusiana na hali ya hewa na maji yamesababisha vifo vya zaidi ya watu milioni mbili huku asilimia 90 kati yao ni katika nchi zinazoendelea.Na ingawa mataifa 108 sasa yana mifumo ya tahadhari za majanga mchanganyiko, shirika hilo linasema viwango vya vifo bado ni mara sita zaidi katika maeneo yasiyo na mifumo hiyo.WMO inasema teknolojia mpya ikiwemo akili mnemba na matumizi ya takwimu za setilaiti kwa wakati halisi zinabadilisha uwezo wa utabiri, lakini pengo la kidijitali bado linawaacha wengi wakiwa hatarini.“Mafanikio ya Tahadhari za Mapema kwa Wote hayapimwi kwa ripoti au maazimio, anasema Celesto bali kwa maisha yanayookolewa na riziki zinazolindwa. Tunapoelekea mwaka 2027, hebu tuongeze juhudi kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa bila ulinzi.”Mkutano huo Maalum wa WMO utaendelea wiki nzima mjini Geneva, huku Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres akitarajiwa kuhutubia siku ya Jumatano.Shirika la WMO wakati likiadhimisha miaka 75 ya kile linachoita Sayansi kwa Vitendo linataka kuhakikisha sayansi hiyo inawafikia wote, kabla ya majanga kutokea.

Duration:00:03:29

Ask host to enable sharing for playback control

20 OKTOBA 2025

10/20/2025
Karibu kusikiliza jarida la habari za Umoja wa Mataifa, leo utasikia mengi ikiwemo mkutano wa kujadili kuhusu tahadhari za mapema unaoenda sambamba na miaka 75 tangu kuanzishwa kwa shirika la Umoja wa Mataifa la hali ya hewa WMO. Pia utasikia juhudi za mashirika ya UN kusaidia wananchi huko mashinani na kuboresha maisha yao. UNDP nchini Tanzania na UNMISS huko jimboni Yambui nchini Sudan Kusini. Mtangazaji wako ni Leah Mushi.

Duration:00:09:59

Ask host to enable sharing for playback control

Mradi wa UNDP na wadau wake wawasaidia wananchi kuondokana na umasikini

10/17/2025
Mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia mbali na kusaidia wananchi kwenye kilimo pia umewawezesha kiuchumi na kuwaondoa baadhi yao kwenye mstari wa umasikini. Mmoja wa walio utupa mkono umasikini ni Judith Mabeta aliyetoka kuishi nyumba ya udongo mpaka kuwa na nyumba ya kupangisha na sasa ni mama mwenye nyumba. Leah Mushi anatujuza zaidi.

Duration:00:02:34

Ask host to enable sharing for playback control

Msaada wa UNICEF waokoa manusura wa mafuriko Magharibi mwa Kenya

10/17/2025
Kupitia msaada wa fedha kutoka Ufaransa, juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya, hasa kwa jamii zilizo katika mazingira hatarishi zinaendelea ambapo juhudi za hivi karibuni ni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya ambao kwa pamoja wameimarisha huduma hizo kwa manusura wa mafuriko Magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Huduma hizi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha watoto na familia wanapata vyakula vyenye virutubishi kwa ustawi wa maisha yao. Sheilah Jengetich na taarifa zaidi kupitia video ya UNICEF Kenya.

Duration:00:03:10

Ask host to enable sharing for playback control

17 OKTOBA 2025

10/17/2025
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNDP ya umaskini, mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia na juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya.Takribani watu milioni 887 duniani ambao ni maskini wanaishi kwenye maeneo yanayokumbwa moja kwa moja na madhara manne yasababishwayo na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni joto kali, mafuriko, ukame na uchafuzi wa hewa, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP kwa kushirikiana na wadau. Ripoti inaonesha bayana kuwa hali hiyo inazidi kutwamisha watu hao kwenye hali tete zaidi.Mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia mbali na kusaidia wananchi kwenye kilimo pia umewawezesha kiuchumi na kuwaondoa baadhi yao kwenye mstari wa umasikini. Mmoja wa walio utupa mkono umasikini ni Judith Mabeta aliyetoka kuishi nyumba ya udongo mpaka kuwa na nyumba ya kupangisha na sasa ni mama mwenye nyumba.Kupitia msaada wa fedha kutoka Ufaransa, juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya, hasa kwa jamii zilizo katika mazingira hatarishi zinaendelea ambapo juhudi za hivi karibuni ni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya ambao kwa pamoja wameimarisha huduma hizo kwa manusura wa mafuriko Magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Huduma hizi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha watoto na familia wanapata vyakula vyenye virutubishi kwa ustawi wa maisha yao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Duration:00:10:25

Ask host to enable sharing for playback control

Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yazidi kutwamisha hali za maskini duniani

10/17/2025
Takribani watu milioni 887 duniani ambao ni maskini wanaishi kwenye maeneo yanayokumbwa moja kwa moja na madhara manne yasababishwayo na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni joto kali, mafuriko, ukame na uchafuzi wa hewa, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP kwa kushirikiana na wadau. Ripoti inaonesha bayana kuwa hali hiyo inazidi kutwamisha watu hao kwenye hali tete zaidi. Assumpta Massoi amepitia ripoti hiyo na kuandaa taarifa hii.

Duration:00:02:37

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana za neno "KIMWA"

10/16/2025
Katika kujifunza Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "KIMWA."

Duration:00:00:49

Ask host to enable sharing for playback control

16 OKTOBA 2025

10/16/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya chakula duniani ikienda sambamba na maadhimisho ya miaka 80 ya kuanzishwa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, na utamsikia Mwakilishi wa FAO nchini Tanzania Bi. Nyabenyi Tito Tipo akieleza.Maadhimisho ya siku ya chakula duniani yamefanyika kimataifa leo huko Roma nchini Italia, yakienda sambamba na sikukuu ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na kilimo, FAO. Katika ujumbe wake alioutoa kwa njia ya video Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema, “Miaka themanini iliyopita, katika dunia iliyosambaratishwa kwa vita, nchi zilikutana kukabiliana na njaa. Miongo kadhaa tangu wakati huo, dunia imepiga hatua kubwa. Lakini bado majanga yanyoonesha kuwa hatuwezi kubweteka iwapo tunataka kuendeleza mafanikio tuliyopata. Tuna mbinu, ufahamu, rasilimali za kutokomeza njaa, na kupatia kila mtu chakula kizuri na chenye afya. Tunachohitaji ni umoja.Huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, raia wamerejea kufuatia makubaliano ya sitisho la mapigano lakini wanahaha kujenga upya makazi yao huku wakiwa wamezingirwa na vifusi. Miongoni mwao Ayman Awadallah, amesema “hakuna maji, hakuna miundombinu ya majitaka, hakuna maisha hapa, hakuna chochote.”Na kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, kilichotokea Jumatano Oktoba 15 nchini India, Umoja wa Mataifa kupitia Katibu Mkuu umetuma salamu za rambirambi na kusema hayati Odinga, alikuwa mtu muhimu katika maendeleo ya kidemokrasia nchini Kenya na pia mtetezi thabiti wa mageuzi ya kikatiba na utawala jumuishi.Na katika kujifunza Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "KIMWA"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Duration:00:13:01

Ask host to enable sharing for playback control

Wanawake wa vijijini nchini Kenya wataka uwezeshaji wa kifedha

10/15/2025
Kuanzia Oktoba 15 mwaka 2008 dunia imekuwa ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini kama fursa ya kutambua mchango mkubwa wa wanawake hawa katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kimazingira.. Sheilah Jepngetich amefuatilia mchango wa wanawake wa vijijini nchini Kenya na kutuandalia taarifa hii.

Duration:00:02:38

Ask host to enable sharing for playback control

Kiwango cha hewa ukaa angani kimefurutu ada na kutishia ongezeko la joto duniani - WMO Ripoti

10/15/2025
Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani, WMO, inasema kiwango cha gesi ya hewa ukaa, yaani carbon dioxide au CO₂, kimeongezeka kwa kiwango cha kuvunja rekodi mwaka 2024, na kufikia viwango vipya vya juu zaidi kuwahi kurekodiwa. Flora Nducha ameisoma ripoti hiyo na anatupa tathimini

Duration:00:03:31

Ask host to enable sharing for playback control

15 OKTOBA 2025

10/15/2025
Hii leo jaridani tunaangazia kiwango cha gesi ya hewa ukaa, yaani carbon dioxide au CO₂, siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini inayotupeleka nchini Kenya kumulika juhudi za wanawake za kumudu mahitaji ya familia zao, na uvuvi na uhalifu katika Ziwa Victoria.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani, WMO, inasema kiwango cha gesi ya hewa ukaa, yaani carbon dioxide au CO₂, kimeongezeka kwa kiwango cha kuvunja rekodi mwaka 2024, na kufikia viwango vipya vya juu zaidi kuwahi kurekodiwa.Kuanzia Oktoba 15 mwaka 2008 dunia imekuwa ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini kama fursa ya kutambua mchango mkubwa wa wanawake hawa katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kimazingira.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM kwa kushirikiana na Ofisi ya Marekani ya Masuala ya Kimataifa ya kupambana na Dawa za Kulevya na Utekelezaji wa Sheria (INL), na mamlaka kutoka Kenya, Tanzania na Uganda wanashirikiana kuimarisha uwezo na kukabiliana na uhalifu wa kimataifa unaotekelezwa katika ziwa victori ambao ukiachwa unaweza kuleta athari kwa zaidi ya watu milioni 40 wanaotegemea ziwa hilo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:10:47

Ask host to enable sharing for playback control

IOM na wadau Kenya waimarisha ulinzi ziwa Victoria kupambana na wahalifu

10/15/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM kwa kushirikiana na Ofisi ya Marekani ya Masuala ya Kimataifa ya kupambana na Dawa za Kulevya na Utekelezaji wa Sheria (INL), na mamlaka kutoka Kenya, Tanzania na Uganda wanashirikiana kuimarisha uwezo na kukabiliana na uhalifu wa kimataifa unaotekelezwa katika ziwa victori ambao ukiachwa unaweza kuleta athari kwa zaidi ya watu milioni 40 wanaotegemea ziwa hilo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi

Duration:00:02:47

Ask host to enable sharing for playback control

Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MKWECHE"!

10/14/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWECHE"!

Duration:00:01:03

Ask host to enable sharing for playback control

14 OKTOBA 2025

10/14/2025
Hii leo jaridani tnakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya Mwalimu Nyerere na tunakupeleka nchini Tanzania ambako kunaendelea juhudi za kuimarisha matumimizi ya lugha ya Kiswahili na utangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashairki, manufaa ya kiuchumi na kijami na kuenzi mchango wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Umoja wa Mataifa leo umeonya kwamba Gaza itahitaji karibu dola bilioni 70 kwa ajili ya ujenzi upya baada ya miaka miwili ya mzozo, huku dola bilioni 20 zikitakiwa katika miaka mitatu ijayo. Makadirio haya yanatokana na, tathmini ya pamoja kati ya Umoja wa Mataifa, Muungano wa Ulaya, na Benki ya Dunia. Mwakilishi Maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP kwa ajili ya programu za msaada kwa Wapalestina Jaco Cilliers,amesema “Viwango vya uharibifu sasa vimefikia karibu asilimia 84, na katika baadhi ya sehemu za Jiji la Gaza, ni hadi asilimia 92.”Umoja wa Mataifa umeongeza hatua zake za dharura huko Gaza kwa kutoa dola milioni 11 kutoka Mfuko wake wa Dharura (CERF) kukidhi mahitaji ya haraka kabla ya kuanza kwa msimu wa baridi. Mgao huu, uliozinduliwa na Mratibu wa Misaada ya Dharura Tom Fletcher, utaunga mkono utoaji wa chakula, maji, huduma za afya na makazi kwa raia walioathiriwa na mzozo wa miaka miwili. Hatua hii inafuatia mgao wa dola milioni 9 wiki iliyopita kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa hospitali na huduma muhimu, na kufanya jumla ya msaada wa hivi karibuni kufikia dola milioni 20.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limeonya kuhusu ongezeko la magonjwa ya neva duniani, ambayo sasa yanachangia zaidi ya vifo milioni 11 kila mwaka. Ripoti mpya ya WHO iliyotolewa leo mjini Geneva inaonesha kuwa zaidi ya watu bilioni 3 sawa na zaidi ya asilimia 40 ya watu duniani wanaishi na magonjwa yanayoathiri ubongo, ikiwemo kiharusi, ugonjwa wa kusahau, kifafa, na maumivu ya kichwa ya muda mrefu. Kwa mujibu wa ripoti nchi maskini ndizo zinazoathirika zaidi, zikiwa na upungufu mara 80 wa idadi ya wataalamu wa magonjwa ya neva ikilinganishwa na nchi tajiri. WHO inazitaka serikali kutoa kipaumbele kwa afya ya ubongo, kuongeza fedha na kuboresha upatikanaji wa huduma za tiba."Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWECHE!Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Duration:00:11:27

Ask host to enable sharing for playback control

Mateka waachiliwa Gaza, misaada yaanza kuingia - UN

10/13/2025
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, leo amekaribisha kwa furaha kuachiliwa kwa mateka wote waliokuwa hai kutoka Gaza, huku mashirika ya misaada yakiripoti kwamba usambazaji wa misaada ya kuokoa maisha sasa unafanyika na misaada inaingia kwa kiwango kikubwa katika eneo hilo lililoharibiwa vibaya na vita: Flora Nducha amefuatilia na hii hapa taarifa yake

Duration:00:02:56

Ask host to enable sharing for playback control

Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike Tanzania

10/13/2025
Tarehe 11 mwezi Oktoba kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, ikiwa ni siku muhimu ya kutambua mchango na uwezo wa mabinti katika jamii. Huko nchini Tanzania, kumefanyika hafla ya maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Plan International Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), na lile linalojishughulisha na Masuala ya Wanawake (UN Women). Sabrina Moshi na taarifa zaidi

Duration:00:02:14

Ask host to enable sharing for playback control

13 OKTOBA 2025

10/13/2025
Hii leo jaridani tunaangazia sitisho la mapigano Gaza na kurejeshwa kwa mateka wote, matumizi ya fecha za umma nchini Tanzania, na Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo uliadhimishwa tarehe 11 mwezi huu.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, leo amekaribisha kwa furaha kuachiliwa kwa mateka wote waliokuwa hai kutoka Gaza, huku mashirika ya misaada yakiripoti kwamba usambazaji wa misaada ya kuokoa maisha sasa unafanyika na misaada inaingia kwa kiwango kikubwa katika eneo hilo lililoharibiwa vibaya na vita.Licha ya mabilioni ya fedha kutumika katika sekta za elimu, afya na miundombinu, mataifa mengi bado yanashindwa kufikia maendeleo ya maana. Swali ni je, suluhisho ni kutumia fedha zaidi, au kuzitumia vyema? Benki ya dunia inatoa jibu kwa swali hilo tuungane na Leah Mushi akitujuza wamesema nini.Tarehe 11 mwezi Oktoba kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, ikiwa ni siku muhimu ya kutambua mchango na uwezo wa mabinti katika jamii. Huko nchini Tanzania, kumefanyika hafla ya maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Plan International Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), na lile linalojishughulisha na Masuala ya Wanawake (UN Women)."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Duration:00:09:51

Ask host to enable sharing for playback control

Wataalamu washauri serikali kutumia teknolojia na takwimu kuboresha utoaji huduma kwa wananchi

10/13/2025
Licha ya mabilioni ya fedha kutumika katika sekta za elimu, afya na miundombinu, mataifa mengi bado yanashindwa kufikia maendeleo ya maana. Swali ni je, suluhisho ni kutumia fedha zaidi, au kuzitumia vyema? Benki ya dunia inatoa jibu kwa swali hilo tuungane na Leah Mushi akitujuza wamesema nini.

Duration:00:02:44