
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
United Nations
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Location:
New Rochelle, NY
Genres:
News & Politics Podcasts
Networks:
United Nations
Description:
Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
Twitter:
@HabarizaUN
Language:
Swahili
Contact:
9178215291
Episodes
Mradi wa UNDP na wadau wake wawasaidia wananchi kuondokana na umasikini
10/17/2025
Mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia mbali na kusaidia wananchi kwenye kilimo pia umewawezesha kiuchumi na kuwaondoa baadhi yao kwenye mstari wa umasikini. Mmoja wa walio utupa mkono umasikini ni Judith Mabeta aliyetoka kuishi nyumba ya udongo mpaka kuwa na nyumba ya kupangisha na sasa ni mama mwenye nyumba. Leah Mushi anatujuza zaidi.
Duration:00:02:34
Msaada wa UNICEF waokoa manusura wa mafuriko Magharibi mwa Kenya
10/17/2025
Kupitia msaada wa fedha kutoka Ufaransa, juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya, hasa kwa jamii zilizo katika mazingira hatarishi zinaendelea ambapo juhudi za hivi karibuni ni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya ambao kwa pamoja wameimarisha huduma hizo kwa manusura wa mafuriko Magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Huduma hizi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha watoto na familia wanapata vyakula vyenye virutubishi kwa ustawi wa maisha yao. Sheilah Jengetich na taarifa zaidi kupitia video ya UNICEF Kenya.
Duration:00:03:10
17 OKTOBA 2025
10/17/2025
Hii leo jaridani tunaangazia ripoti ya UNDP ya umaskini, mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia na juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya.Takribani watu milioni 887 duniani ambao ni maskini wanaishi kwenye maeneo yanayokumbwa moja kwa moja na madhara manne yasababishwayo na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni joto kali, mafuriko, ukame na uchafuzi wa hewa, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP kwa kushirikiana na wadau. Ripoti inaonesha bayana kuwa hali hiyo inazidi kutwamisha watu hao kwenye hali tete zaidi.Mradi wa kusaidia jamii kupambana na athari za mabadiliko ya tabianchi nchini Zambia mbali na kusaidia wananchi kwenye kilimo pia umewawezesha kiuchumi na kuwaondoa baadhi yao kwenye mstari wa umasikini. Mmoja wa walio utupa mkono umasikini ni Judith Mabeta aliyetoka kuishi nyumba ya udongo mpaka kuwa na nyumba ya kupangisha na sasa ni mama mwenye nyumba.Kupitia msaada wa fedha kutoka Ufaransa, juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya, hasa kwa jamii zilizo katika mazingira hatarishi zinaendelea ambapo juhudi za hivi karibuni ni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya ambao kwa pamoja wameimarisha huduma hizo kwa manusura wa mafuriko Magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Huduma hizi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha watoto na familia wanapata vyakula vyenye virutubishi kwa ustawi wa maisha yao.Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Duration:00:10:25
Madhara ya mabadiliko ya tabianchi yazidi kutwamisha hali za maskini duniani
10/17/2025
Takribani watu milioni 887 duniani ambao ni maskini wanaishi kwenye maeneo yanayokumbwa moja kwa moja na madhara manne yasababishwayo na mabadiliko ya tabianchi ambayo ni joto kali, mafuriko, ukame na uchafuzi wa hewa, imesema ripoti mpya iliyotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP kwa kushirikiana na wadau. Ripoti inaonesha bayana kuwa hali hiyo inazidi kutwamisha watu hao kwenye hali tete zaidi. Assumpta Massoi amepitia ripoti hiyo na kuandaa taarifa hii.
Duration:00:02:37
Jifunze Kiswahili: Maana za neno "KIMWA"
10/16/2025
Katika kujifunza Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "KIMWA."
Duration:00:00:49
16 OKTOBA 2025
10/16/2025
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya chakula duniani ikienda sambamba na maadhimisho ya miaka 80 ya kuanzishwa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO, na utamsikia Mwakilishi wa FAO nchini Tanzania Bi. Nyabenyi Tito Tipo akieleza.Maadhimisho ya siku ya chakula duniani yamefanyika kimataifa leo huko Roma nchini Italia, yakienda sambamba na sikukuu ya miaka 80 tangu kuanzishwa kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na kilimo, FAO. Katika ujumbe wake alioutoa kwa njia ya video Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amesema, “Miaka themanini iliyopita, katika dunia iliyosambaratishwa kwa vita, nchi zilikutana kukabiliana na njaa. Miongo kadhaa tangu wakati huo, dunia imepiga hatua kubwa. Lakini bado majanga yanyoonesha kuwa hatuwezi kubweteka iwapo tunataka kuendeleza mafanikio tuliyopata. Tuna mbinu, ufahamu, rasilimali za kutokomeza njaa, na kupatia kila mtu chakula kizuri na chenye afya. Tunachohitaji ni umoja.Huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa na Israeli, raia wamerejea kufuatia makubaliano ya sitisho la mapigano lakini wanahaha kujenga upya makazi yao huku wakiwa wamezingirwa na vifusi. Miongoni mwao Ayman Awadallah, amesema “hakuna maji, hakuna miundombinu ya majitaka, hakuna maisha hapa, hakuna chochote.”Na kufuatia kifo cha aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga, kilichotokea Jumatano Oktoba 15 nchini India, Umoja wa Mataifa kupitia Katibu Mkuu umetuma salamu za rambirambi na kusema hayati Odinga, alikuwa mtu muhimu katika maendeleo ya kidemokrasia nchini Kenya na pia mtetezi thabiti wa mageuzi ya kikatiba na utawala jumuishi.Na katika kujifunza Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "KIMWA"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!
Duration:00:13:01
Wanawake wa vijijini nchini Kenya wataka uwezeshaji wa kifedha
10/15/2025
Kuanzia Oktoba 15 mwaka 2008 dunia imekuwa ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini kama fursa ya kutambua mchango mkubwa wa wanawake hawa katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kimazingira.. Sheilah Jepngetich amefuatilia mchango wa wanawake wa vijijini nchini Kenya na kutuandalia taarifa hii.
Duration:00:02:38
Kiwango cha hewa ukaa angani kimefurutu ada na kutishia ongezeko la joto duniani - WMO Ripoti
10/15/2025
Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani, WMO, inasema kiwango cha gesi ya hewa ukaa, yaani carbon dioxide au CO₂, kimeongezeka kwa kiwango cha kuvunja rekodi mwaka 2024, na kufikia viwango vipya vya juu zaidi kuwahi kurekodiwa. Flora Nducha ameisoma ripoti hiyo na anatupa tathimini
Duration:00:03:31
15 OKTOBA 2025
10/15/2025
Hii leo jaridani tunaangazia kiwango cha gesi ya hewa ukaa, yaani carbon dioxide au CO₂, siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini inayotupeleka nchini Kenya kumulika juhudi za wanawake za kumudu mahitaji ya familia zao, na uvuvi na uhalifu katika Ziwa Victoria.Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa Duniani, WMO, inasema kiwango cha gesi ya hewa ukaa, yaani carbon dioxide au CO₂, kimeongezeka kwa kiwango cha kuvunja rekodi mwaka 2024, na kufikia viwango vipya vya juu zaidi kuwahi kurekodiwa.Kuanzia Oktoba 15 mwaka 2008 dunia imekuwa ikiadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake wa Vijijini kama fursa ya kutambua mchango mkubwa wa wanawake hawa katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi, na kimazingira.Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM kwa kushirikiana na Ofisi ya Marekani ya Masuala ya Kimataifa ya kupambana na Dawa za Kulevya na Utekelezaji wa Sheria (INL), na mamlaka kutoka Kenya, Tanzania na Uganda wanashirikiana kuimarisha uwezo na kukabiliana na uhalifu wa kimataifa unaotekelezwa katika ziwa victori ambao ukiachwa unaweza kuleta athari kwa zaidi ya watu milioni 40 wanaotegemea ziwa hilo.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:10:47
IOM na wadau Kenya waimarisha ulinzi ziwa Victoria kupambana na wahalifu
10/15/2025
Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji IOM kwa kushirikiana na Ofisi ya Marekani ya Masuala ya Kimataifa ya kupambana na Dawa za Kulevya na Utekelezaji wa Sheria (INL), na mamlaka kutoka Kenya, Tanzania na Uganda wanashirikiana kuimarisha uwezo na kukabiliana na uhalifu wa kimataifa unaotekelezwa katika ziwa victori ambao ukiachwa unaweza kuleta athari kwa zaidi ya watu milioni 40 wanaotegemea ziwa hilo. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Leah Mushi
Duration:00:02:47
Jifunze Kiswahili: Maana ya neno "MKWECHE"!
10/14/2025
Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWECHE"!
Duration:00:01:03
14 OKTOBA 2025
10/14/2025
Hii leo jaridani tnakuletea mada kwa kina inayoangazia siku ya Mwalimu Nyerere na tunakupeleka nchini Tanzania ambako kunaendelea juhudi za kuimarisha matumimizi ya lugha ya Kiswahili na utangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashairki, manufaa ya kiuchumi na kijami na kuenzi mchango wa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.Umoja wa Mataifa leo umeonya kwamba Gaza itahitaji karibu dola bilioni 70 kwa ajili ya ujenzi upya baada ya miaka miwili ya mzozo, huku dola bilioni 20 zikitakiwa katika miaka mitatu ijayo. Makadirio haya yanatokana na, tathmini ya pamoja kati ya Umoja wa Mataifa, Muungano wa Ulaya, na Benki ya Dunia. Mwakilishi Maalum wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP kwa ajili ya programu za msaada kwa Wapalestina Jaco Cilliers,amesema “Viwango vya uharibifu sasa vimefikia karibu asilimia 84, na katika baadhi ya sehemu za Jiji la Gaza, ni hadi asilimia 92.”Umoja wa Mataifa umeongeza hatua zake za dharura huko Gaza kwa kutoa dola milioni 11 kutoka Mfuko wake wa Dharura (CERF) kukidhi mahitaji ya haraka kabla ya kuanza kwa msimu wa baridi. Mgao huu, uliozinduliwa na Mratibu wa Misaada ya Dharura Tom Fletcher, utaunga mkono utoaji wa chakula, maji, huduma za afya na makazi kwa raia walioathiriwa na mzozo wa miaka miwili. Hatua hii inafuatia mgao wa dola milioni 9 wiki iliyopita kwa ajili ya kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa hospitali na huduma muhimu, na kufanya jumla ya msaada wa hivi karibuni kufikia dola milioni 20.Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO limeonya kuhusu ongezeko la magonjwa ya neva duniani, ambayo sasa yanachangia zaidi ya vifo milioni 11 kila mwaka. Ripoti mpya ya WHO iliyotolewa leo mjini Geneva inaonesha kuwa zaidi ya watu bilioni 3 sawa na zaidi ya asilimia 40 ya watu duniani wanaishi na magonjwa yanayoathiri ubongo, ikiwemo kiharusi, ugonjwa wa kusahau, kifafa, na maumivu ya kichwa ya muda mrefu. Kwa mujibu wa ripoti nchi maskini ndizo zinazoathirika zaidi, zikiwa na upungufu mara 80 wa idadi ya wataalamu wa magonjwa ya neva ikilinganishwa na nchi tajiri. WHO inazitaka serikali kutoa kipaumbele kwa afya ya ubongo, kuongeza fedha na kuboresha upatikanaji wa huduma za tiba."Na katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "MKWECHE!Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:11:27
Mateka waachiliwa Gaza, misaada yaanza kuingia - UN
10/13/2025
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, leo amekaribisha kwa furaha kuachiliwa kwa mateka wote waliokuwa hai kutoka Gaza, huku mashirika ya misaada yakiripoti kwamba usambazaji wa misaada ya kuokoa maisha sasa unafanyika na misaada inaingia kwa kiwango kikubwa katika eneo hilo lililoharibiwa vibaya na vita: Flora Nducha amefuatilia na hii hapa taarifa yake
Duration:00:02:56
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike Tanzania
10/13/2025
Tarehe 11 mwezi Oktoba kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, ikiwa ni siku muhimu ya kutambua mchango na uwezo wa mabinti katika jamii. Huko nchini Tanzania, kumefanyika hafla ya maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Plan International Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), na lile linalojishughulisha na Masuala ya Wanawake (UN Women). Sabrina Moshi na taarifa zaidi
Duration:00:02:14
13 OKTOBA 2025
10/13/2025
Hii leo jaridani tunaangazia sitisho la mapigano Gaza na kurejeshwa kwa mateka wote, matumizi ya fecha za umma nchini Tanzania, na Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike ambayo uliadhimishwa tarehe 11 mwezi huu.Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, leo amekaribisha kwa furaha kuachiliwa kwa mateka wote waliokuwa hai kutoka Gaza, huku mashirika ya misaada yakiripoti kwamba usambazaji wa misaada ya kuokoa maisha sasa unafanyika na misaada inaingia kwa kiwango kikubwa katika eneo hilo lililoharibiwa vibaya na vita.Licha ya mabilioni ya fedha kutumika katika sekta za elimu, afya na miundombinu, mataifa mengi bado yanashindwa kufikia maendeleo ya maana. Swali ni je, suluhisho ni kutumia fedha zaidi, au kuzitumia vyema? Benki ya dunia inatoa jibu kwa swali hilo tuungane na Leah Mushi akitujuza wamesema nini.Tarehe 11 mwezi Oktoba kila mwaka dunia huadhimisha Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Kike, ikiwa ni siku muhimu ya kutambua mchango na uwezo wa mabinti katika jamii. Huko nchini Tanzania, kumefanyika hafla ya maadhimisho hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Plan International Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wakiwemo Ofisi za Umoja wa Mataifa Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF), na lile linalojishughulisha na Masuala ya Wanawake (UN Women)."Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!
Duration:00:09:51
Wataalamu washauri serikali kutumia teknolojia na takwimu kuboresha utoaji huduma kwa wananchi
10/13/2025
Licha ya mabilioni ya fedha kutumika katika sekta za elimu, afya na miundombinu, mataifa mengi bado yanashindwa kufikia maendeleo ya maana. Swali ni je, suluhisho ni kutumia fedha zaidi, au kuzitumia vyema? Benki ya dunia inatoa jibu kwa swali hilo tuungane na Leah Mushi akitujuza wamesema nini.
Duration:00:02:44
Puja ya Durga nchini India, ambako ibada hukutana na mabadiliko ya kijamii
10/10/2025
Mnamo mwaka wa 2021, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) liliongeza kwenye orodha ya turathi za dunia za tamaduni zisizoshikika au kugusika, Puja Durga ambayo ni sherehe kubwa ya kihindu ya ushindi wa mungu wa kike aitwaye Durga dhidi ya jini Mahishasura, ikiwa ni ishara ya ushindi wa mema dhidi ya maovu. Assumpta Massoi na maelezo zaidi.
Duration:00:04:09
Maria Corina Machado ndiye mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel 2025, anatoka Venezuela, UN yampongeza
10/10/2025
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) imekaribisha uamuzi wa Kamati ya Tuzo ya Amani ya Nobel kumtangaza Maria Corina Machado kiongozi wa upinzani nchini Venezuela kuwa mshindi wa mwaka huu wa tuzo ya amani ya Nobel, kwa kutambua kazi yake ya kuendeleza matumaini ya demokrasia ya watu wa Venezuela. Flora Nducha na maelezo zaidi.
Duration:00:03:16
10 OKTOBA 2025
10/10/2025
Hii leo jaridani tunaangazia mshindi wa mwaka huu wa tuzo ya amani ya Nobel, sauti za wanawake nchini Kenya ambazo zimeanza kusikika kwa uthabiti, zikililia haki, heshima, na usawa, na Puja Durga ambayo ni sherehe kubwa ya kihindu ya ushindi wa mungu wa kike.Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu (OHCHR) imekaribisha uamuzi wa Kamati ya Tuzo ya Amani ya Nobel kumtangaza Maria Corina Machado kiongozi wa upinzani nchini Venezuela kuwa mshindi wa mwaka huu wa tuzo ya amani ya Nobel, kwa kutambua kazi yake ya kuendeleza matumaini ya demokrasia ya watu wa Venezuela.Katika kila kona ya Kenya, sasa sauti za wanawake zimeanza kusikika kwa uthabiti, zikililia haki, heshima, na usawa. Kupitia msaada wa mashirika ya kimataifa kama shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), mabadiliko yanaanza kushika kasi.Mnamo mwaka wa 2021, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) liliongeza kwenye orodha ya turathi za dunia za tamaduni zisizoshikika au kugusika, Puja Durga ambayo ni sherehe kubwa ya kihindu ya ushindi wa mungu wa kike aitwaye Durga dhidi ya jini Mahishasura, ikiwa ni ishara ya ushindi wa mema dhidi ya maovu"Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Duration:00:10:38
UNDP na UNODC yafanikisha usawa wa kijinsia kwa wanawake nchini Kenya
10/10/2025
Katika kila kona ya Kenya, sasa sauti za wanawake zimeanza kusikika kwa uthabiti, zikililia haki, heshima, na usawa. Kupitia msaada wa mashirika ya kimataifa kama shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendeleo, UNDP na Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kupambana na dawa za Kulevya na Uhalifu(UNODC), mabadiliko yanaanza kushika kasi. Katika jamii ambazo kwa muda mrefu mifumo ya jadi na taasisi za kisheria zimewabagua au kuwapuuza wanawake Taarifa ya SHEILAH Jepngetich inafafanua zaidi
Duration:00:03:06